Karibu Nyumbani - Tunaipenda Tanzania

SIKILIZA HAPA JIBAMBEE RADIO SHOW

Latest Articles

September 20, 2017

Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.

Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.
Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.

Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.

Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
Stori na BBC
Continue reading

Msanii wa Bongo Flava, Barnaba ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Mapenzi Jeneza’, video imeongozwa na Joowzey. Itupie macho hapo chini>>>
Continue reading

Msanii Wizkid ameachia wimbo wake mpya ‘Everytime’ ambao amemshirikisha rapper Future kutoka Marekani. 

Mpaka sasa tayari Wizkid ameshafanya kazi na mastaa kadhaa wa Marekani akiwemo Chris Brown, Drake na Ty Dolla $ign. Usikilize hapa chini wimbo huo.
Continue reading

Wiki hii katika Exclusive Interview kutoka Asili TV Online, reporter wetu kutoka Arusha Stanley Lema amepiga stori na Daniel Meshack ambaye ni mtaalamu wa sanaa ya kuchonga vinyago na kazi nyingine za mikono katika Maasai Market Arusha.

Wamezungumza vitu "tuwe na uzalendo wa vitu vyetu vya nyumbani, kwasababu wao wamevipenda vya kwetu">>> Daniel Meshack
Msikilize hapo chini na kisha tupe maoni yako.
Continue reading

September 19, 2017

Staa wa muziki kutoka nchini Marekani maarufu kama Lady Gaga, 31, kwa taarifa zilizopo kwa sasa yuko katika wakati mgumu kutokana na maradhi yanayomsababishia maumivu makali.
Staa huyo wa wimbo wa 'Johanne' amelazimika kuahirisha ziara yake ya muziki iliyokuwa ifanyike Septemba 21, Barcelona, Uispania na kusogezwa mbele hadi mwakani 2018.

Hii ikiwa ni kutokana na kuhisi maumivu makali, ambapo sasa kwa mujibu wa hollywoodlife, Lady Gaga yuko katika uangalizi wa wataalamu wa kiafya.
Continue reading

Staa wa muziki kutoka Marekani maarufu kama Selena Gomez kupitia account yake ya Instagram amethibitisha kula shavu na kampuni kubwa duniani ya PUMA.

Selena juzi kati alikabiliwa na kufanyiwa upasuaji kutokana na kupatwa na tatizo la figo, hata hivyo tatizo hilo limeweza kumuacha salama na sasa amepiga mchongo na kampuni ya mavazi, viatu na vifaa kibao vya PUMA.
Continue reading

Msanii wa muziki kutoka Uingereza Rita Ora, aliyewahi kuwa katika label ya Jay Z Rock Nation, amedondosha video yake inayokwenda kwa jila la 'Lonely Together', Itizame hapo chini>>>
Continue reading

Msanii aliyewahi kufanya kazi na wasanii kibao akiwemo Kanye West na Lady Gaga, unaweza muita Sam Bruno sasa amedondosha wimbo wake binafsi unaozidi kuwashika mashabiki wake, wimbo unaitwa 'Hello Hater'.

Unajua jina la huu wimbo lilikujaje? Msanii huyu alikuwa studio na wenzake, wakati ameshika mic aki freestyle mara akaimba hivi “They never, never shut up,” mara wenzeke wakaitikia, ‘Hey, haters never shut up, mara msanii huyo akaona mbona huu ndo mchongo, basi sawa.” I was like, “Perfect!”

Sikiliza wimbo wake mpya hapo chini>>>
Continue reading

September 18, 2017

Mmoja kati ya wakongwe wa muziki wa kizazi kipya nchini maarufu kama Jay Moe amekuletea video yake mpya ya wimbo wa Me &You, aliomshirikisha msanii Ke'miller, tazama video hiyo hapo chini>>>
Continue reading

Mkali wa miondoko ya singeli Man Fongo sasa amekusogezea wimbo wake unaitwa 'SIO POA' audio na video ziko hapa>>>bonyeza DOWNLOAD kwa Audio na Video hapo chini>>>
Continue reading

Msanii wa Bongo Fleva, Hemedy Phd ameachia video ya ngoma yake mpya ‘Mkimbie’ kichupa kimeongozwa na Khalfani khalmandro na audio imetengenezwa Sei Records. Tazama video hapa chini>>>

Continue reading

Nahodha wa zamani wa kikosi cha England Wayne Rooney amefika mahakamani na kukiri kuendesha gari akiwa mlevi.

Alikamatwa wakati polisi walisimamisha gari lake huko Wilmslow, Cheshire tarehe mosi mwezi Septemba.

Rooney 31 alipigwa marufuku ya kuendesha gari kwa miaka miwili na kuamrishwa kutoa huduma ya jamii bila malipo kwa masaa 100.

Rooney pia aliamrishwa kulipa pauni 170 wakati alifika katika mahakama ya Stockport.

Mzaliwa huyo wa Liverpool alojiunga tena na klabu yake ya utotoni ya Eveton miaka 13 tangu akihame na kuelekea Manchester United.

Baba huyo wa watoto watatu ndiye anayeshikisa rekodi ya kufunga mabao mengi zaidi nchini Uingereza.
Continue reading

 Huenda ukawa wewe ni mmoja ya wale wasiochezea fursa na umekuwa na kiu ya kutaka kupata elimu ya jinsi ya kufuga kuku wa kienyeji.

 Reporter wetu Stanley Lema kutoka Arusha amepiga stori na mtaalamu kutoka Jilala Agrovate Arusha, 'Asanteeli E. Mbisse', msikilize hapa akueleze jinsi ya kuanza ufugaji wa faida kwa kuku wa kienyeji.
Continue reading

September 14, 2017

Karibu wakwetu nikitambulishe kipindi cha redio kwako chenye MATUKIO makubwa yaliyobamba duniani kote kupitia JIBAMBEE RADIO SHOW yetu.

Kuwa wa kwanza kusikiliza kipindi hiki na unaweza kushare katika mtandao wako wa kijamii au unaweza download package zetu ukasikiliza muda wowote nyumbani kwako. 

Fuatilia kipindi hiki kila wiki. Asante kwa kujibamba nasi>>>

Sikiliza hapa chini>>>
Continue reading