HABARI MPYA:

BONGO MUSIC

ENTERTAINMENT

HABARI ZA MASTAA WOTE

HABARI KUTOKA JIJINI ARUSHA ZICHEKI HAPA.

Video Of Day

PICHA ZA WAIGIZAJI WA KIKE WATAKAO ITEKA NOLLYWOOD MWAKA 2012

April 30, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.

1.Nse Ikpe Etim


Tonto Dike

Chelsea Eze

MBONG AMATA

BEVERLY NAYA

OMOTALA JALADE EKEINDE

GENEVIEVE NNAJI

INI OBONG EDO

STELLA DAMASCUS

MIXTAPE MPYA YA AKON 'THE KONCRETE'

April 29, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.


ACTRESS TWINS FROM NOLLYWOOD LEAVE PEOPLE IN DILEMMA

All rights reserved to Asili Yetu.

Enugu celebrity twins, Chidiebere and Chidinma Aneke are no strangers to movie buffs in Nigeria .
 
It is not always common to see twins  who would want to take the same path in life?

We both went into acting because we loved and wanted to act. Before this time, we sat and talked about it. We knew what we were good at doing and it has being fun. At the moment, we are still on top of our games. Acting is our dream and we are happy doing what  we enjoy doing. So, most times, we act twin roles and twin characters. Nigeria has not really reached the stage where one actor can really act twin roles successfully hence, identical twins in that kind of production saves the day.

Have you in the course of acting done twin roles?
Yes, we have done a lot of twin characters and they were great movies.

Tell us a little about the movies you have done together?
We have done Crazy Twins, Jealous Friends, Desperate Twins, Lagos Girls, Broken Ambition, Revenge of the gods and many others.

What do you think can divide the two of you?
Marriage can divide the two of us. But we have prayed to marry twin brothers and that our marriages should take place on the same day. But we say this because we are just humans. God’s will definitely grant us all of our wishes.
You have been praying to marry twins as  you said. Have you ever dated any?

We haven’t seen a reason to  date any perhaps because the ones we have met so far have questionable characters. Sometimes, we noticed that the twin brothers would prefer just one of us. We cannot obviously allow that to happen. We love ourselves so much that we cannot allow men to tear us apart. At the moment, we are waiting for God’s guidance.

We have seen situations where identical twins hate each other to the extent of one taking the life of the other. What do you think is  binding two of you together?

Love is the factor and we cannot imagine death of either of us. The other thing that binds us together is majorly the grace of God.
Have you girls ever switched lovers before?

No! We haven’t . But we have experienced something like that while we were growing up. At that time, the guy asked Chidinma out but she wasn’t interested in him,  we wanted to play games with him, by going for his money.  So, l was always at the guy’s house pretending to be Chidinma while extorting   money from him. This went on until l was nearly raped by the guy in question. But we had to call off the game after that incident.
From then on, we have lived with the principle of not eating what we are not interested in from the beginning.

What happens in a situation where both of you are lucky in terms of meeting Mr. right. May be,Chidebere is lucky, and  Chidinma is not?

My sister knows what’s good for me and likewise, I know what’s good for her. So, if we unfortunately meet two brothers who wish to date us and one of them misbehaves then, we’ll have to call off the relationship with the two brothers. Chidiebere and I were born on the same day. We are identical twins. So we intend to get married on the same day.  I do not want to get married while my twin sister is unmarried. We must get married on the same day.

What if you meet two guys, who are not twins, yet they are responsible and wish to marry you and your twin sister  on the same day?
When that happens then, we ‘ll study them  and talk to God about them. If it is the will of God, why not?

Is that why you are not married yet?
Yes
Are you saying if you do not get men who would marry both of you on the same day, you wouldn’t marry at all?
What we are trying to explain is this: Our dowry can be paid separately, but when it comes to  traditional marriage and the church wedding, we plan to do it on the same day. That’s not too much to ask!


KANYE WEST ABAMBWA AKIPANDISHA NGUO YA NDANI WAKATI AKIWA NA KIM KARDASHIAN

All rights reserved to Asili Yetu.

 
Mchongo huu ulitokea wakati Kanye ametoka kupata chakula cha jioni na bibie Kim Kardashian.Ni kawaida saana kwa kim kupendeza wakati akiwa ametinga suruali taiti ya rather/ngozi.Inasemekana wawili hawa ni mpango mzima na Kanye huenda alikuwa tungi wakati akishuka ndani ya gari suruali aliyokuwa ametupia aina ya rather, koti la blue flani hivi, Tshirt black na boot ya Timberland ni vya ghali sana. Rapa huyo alikuwa akijisogeza katika himaya yake na mtoto Kardashian, wakati inasemekana wamekuwa wakionekana wakila bata pamoja mara kwa mara.DICTIONARY YA MWANAMKE NA MWANAMUME.

Fuatilia vituko vijavyo hapa!

MAISHA YA KIJIJINI HUWA NA VIJIMAMBO NA CHANGAMOTO KAMA HIZI.

April 28, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.

Hii ni nyumba ya msonge ambayo wakazi wa kijiji cha Nyichoka mkoani mara, huitumia kulazia mifugo (Mbuzi)
Kuna aina nyingi sana za maisha, lakini kunaaina kuu mbili  za maisha, nazo ni maisha ya mjini na kijijini.Ni wazi kuwa wakazi wa mjini hutegemea  saana vijijini hasa katika swala zima la mazao. Hakuna ubishi kuwa maisha ya kijijini ni tabu tupu, hasa katika huduma za kijamii kama maji, zahanati, vyombo vya habari, elimu, miundo mbinu na vingine vingi kama imani potofu.

Ukabila nao unachukua kasi kubwa katika jamii kadhaa  huko vijijini, nikitu cha kushangaza mpaka leo makabila flani bado yanajitenga na makabila mengine, ni sawa kwasababu kila kabila lina miiko yao na tamaduni zake. Lakini wahenga walisema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, kisawahili ni nguzo pekee inayounganisha watu wote tokea mwaka wa 1961 wakati Tanganyika ikipata uhuru wake mpaka sasa, hivyo ni vyema watanzania tukaweka tofauti zetu pembeni na kufanya maendeleo.

Huenda leo hii ningepata nafasi ya kuulizwa ungependa nini watu wa kijijini wafanyiwe , basi ningekuwa na meengi ya kueleza, lakini hili pia ni moja wapo; ningepeda baadhi ya vipindi vya Luninga na Redio vipewe udhamini huko ndani kabisa vijijii ambako mpaka leo wananchi wanajua kuwa  Nyerere ndio rais mpaka sasa.

Hiki ni chombo maalum kilichotengenezwa kwa kutumia fito za miti kwaajiri ya kusafirishia mbolea aina ya samadi kwenda shambani.


NEW SONG - TORGIZZLE + NGASEP. FT. CINDY RULZ + Number One (finale).

April 25, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.


STORY KUHUSU MAISHA YA KANUMBA ZAZIDI KUANDIKWA NA VYOMBO MBALI MBALI VYA HABARI.

All rights reserved to Asili Yetu.Msanii wa filamu Elizabeth Maiko (Lulu) akiwa mahakamani.

'JUDGMENT DAY' YA WHITNEY HOUSTON YA IMBWA TENA NA MSANII 'MIRRYCANDLE' KWA KUMUENZI.

All rights reserved to Asili Yetu.
 Mwanadada MirryCandle alodrop video ya "CandleLight" amefanya cover song ya "judgement day" kumuenzi Whitney houston."She was and will forever be my inspiration katika kufaya music!wimbo nimerecord pande za noizmekah.com kama tribute kwake marehem,in loving memory"..

ORODHA YA WABUNGE WALIOWEKA SAHIHI YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU.

April 24, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.

Kiongozi wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe akiweka sahihi katika fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
1.    Mhe. Rashid Ali Abdallah – cuf
2.    Mhe . Chiku Aflah Abwao- chadema
3.    Mhe . Saluim Ali Mbarouk – cuf
4.    Mhe . salum Khalfam Barwany – cuf
5.    Mhe . Deo Haule  Filikuchombe- ccm
6.    Mhe.Pauline Philipo Gekul- chadema
7.    Mhe. Asaa Othman  Hamad-cuf
8.    Mhe. Prof.Kuliyokela Kahigi- Chadema
9.    Mhe.Naomi  Mwakyoma Kaihula – chadema
10.    Mhe . Sylvester Kasulumbayi- chadema
11.    Mhe. Raya Ibrahim Khamis  – chadema
12.    Mhe. Mkiwa Hamad Kiwanga  – cuf
13.    Mhe. Susan  Limbweni Kiwanga- chadema
14.    Mhe. Grace Sindato Kiwelu –chadema
15.    Mhe. Kombo Khamis Kombo – cuf
16.    Mhe. Joshua  Samwel  Nassari – chadema
17.    Mhe. Tundu Antiphas Lissu- chadema
18.    Mhe Aphaxar  Kangi Lugola- ccm
19.    Mhe susan Anselim Lymo- chadema
20.    Mhe. Moses Machali – NCCR Mageuzi
21.    Mhe. John Shibuda Magalle – Chadema
22.    Mhe. Faki  Haji  Makame- Cuf
23.    Mhe . Esther Nicholas Matiko- chadema
24.    Mhe. Joseph Osmund Mbilinyi- Chadema
25.    Mhe. Freman  Aikaeli Mbowe- chadema
26.    Mhe. Kurudhum Jumanne Mchuchuli – chadema
27.    Mhe. Halima James Mdee-chadema
28.    John John Mnyika- Chadema
29.    Mhe. Augustino Lyatonga Mrema- TLP
30.    Mhe . Maryam Salum  Msabaha- chadema
31.    Mhe. Peter Msingwa-chadema
32.    Mhe. Christowaja Gerson Mtinda- chadema
33.    Mhe. Philipa Geofrey Mturano- chadema
34.    Mhe. Christina Lissu Mughwai- chadema
35.    Mhe. Joyce John  Mukya – chadema
36.    Mhe. Mchungaji  Israel  Yohane  Natse – chadema
37.    Mhe. Philemon Ndesamburo- chadema
38.    Mhe. Ahmed  Juma Ngwali- – cuf
39.    Mhe. Vincent  Josephat  Nyerere- chadema
40.    Mhe. Rashid  Ali Omar- cuf
41.    Meshack  Jeremiah Opulukwa- chadema
42.    Mhe. Lucy Philemon Owenya- chadema
43.    Mhe. Rachel Mashishanga- Chadema
44.    Mhe. Mhonga Said Ruhwanya – chadema
45.    Mhe. Conchesta Rwamlaza – Chadema
46.    Mhe. Moza Abedi  Saidy- cuf
47.    Mhe. Joseph  Roman Selasini – Chadema
48.    Mhe. David Ernest  Silinde- chadema
49.    Mhe Rose Kamili Sukum  – chadema
50.    Mhe. Cecilia Daniel Paresso- chadema
51.    Mhe .Kabwe Zuberi Zitto- Kigoma Kaskazini
52.    Mhe. Magdalena Sakaya – Cuf
53.    Mhe Rebecca Mngodo- Cuf
54.    Mhe. Sabreena Sungura -chadema
55.    Mhe. Hamad Rashid Mohammed- CUF
56.    Mhe. Rukia Kassim Ahmed (Cuf)
57.    Mhe. Mustapha Boay Akoonay (Chadema)
58.    Mhe. Abdalla Haji Ali (CUF)
59.    Mhe. Khatibu Said Ali (CUF)
60.    Mhe. Hamad Ali Hamad (CUF)
61.    Mhe. Riziki Omar Juma (CUF)
62.    Mhe  Haji Khatibu  Kai (CUF)
63.    Mhe. Anna Marystella John Malack -Chadema
64.    Mhe. Hamad Rashid Mohamed  (CUF)
65.    Mhe. Rajab Mbarouk Mohamed (CUF)
66.    Mhe. Thuwayba Idrissa Muhamed (CUF)
67.    Mhe. Masoud Abdallah Salum (CUF)
68.    Mhe. Muhamad Ibrahim Sanya (CUF)
69.    Mhe. Ali Khamis Seif (CUF)
70.    Mhe. Haroub Muhammed Shamis (CUF)
71.    Mhe. Amina Amour Nassoro (CUF)  

Na Mpekuzi.

WAZIRI MKUU MIZENGO PINDA AHITIMISHA KIKAO CHA BUNGE KWA KUSEMA HAYA..

All rights reserved to Asili Yetu.


 *ALIPOULIZWA AKACHEKA, MKONO NAE AWEKA SAINI AONDOLEWE, UFISADI MALIASILI UNATISHA
WAKAT
I wabunge wakiendelea kusaini fomu ya majina ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiongozi huyo wa shughuli za Serikali bungeni jana alikwepa kuzungumzia hatua za kinidhamu dhidi ya mawaziri wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Akiahirisha Mkutano wa Saba bungeni Dodoma, Pinda hakugusia suala la kujiuzulu kwa mawaziri wanane na badala yake alisema: “Siku zote Serikali imekuwa tayari kupokea ushauri wa Bunge baada ya kusikiliza mjadala na mapendekezo ya waheshimiwa wabunge.’’

Baada ya kuahirishwa kwa Bunge hadi Juni 12, mwaka huu. Pinda akiwa nje ya Bunge alikwepa kuzungumzia suala hilo licha ya kubanwa na waandishi wa habari na badala yake alicheka: "Haahaa,"  kisha akaingia kwenye gari na kuondoka.

Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe alisema kitendo cha Pinda kushindwa kuzungumzia chochote kuhusu agizo la wabunge kutaka mawaziri wanane wawajibishwe, kimewaacha wananchi katika hofu.

Alisema Waziri Mkuu ametoa hotuba nyepesi kama vile taifa haliko katika giza kutokana na Bunge kutaka kuwajibishwa kwa mawaziri hao na kuapa kulifikisha suala hilo kwa wananchi.

“Aliahirisha shughuli za Bunge kama hakuna kitu kikubwa kilichohitaji majibu ya Serikali, wananchi walitaka kusikia mawaziri waliotajwa kwa tuhuma za ufisadi wakiwajibishwa lakini, hakuna chochote kilichofanyika. Sasa sisi tutakwenda kwa wananachi.

Jumamosi iliyopita, Pinda aliahidi kuwa jana Serikali ingeweka hadharani msimamo wake kuhusu suala baadhi ya mawaziri kutakiwa kujiuzulu lakini hakutekeleza ahadi yake.

Jana, Waziri Mkuu alisema Serikali itachukua hatua stahiki kuimarisha usimamizi na utendaji ndani ya wizara, Serikali za Mitaa na vyombo husika katika kuhakikisha watendaji wake wanafanya kazi kwa umakini.

Mawaziri wazidi kubanwa
Wakati Pinda akikwepa kuzungumzia suala hilo, joto la mawaziri kutakiwa kujiuzulu linazidi kupanda baada ya vigogo zaidi kuendelea kusaini fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani naye huku viongozi wa dini wakisema suala la mawaziri kung’oka ni la lazima.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, viongozi wa dini walisema kuwa suala la mawaziri hao kujiuzulu halina mjadala na kusisitiza kuwa kuwajibika kwa kiongozi kunamjengea heshima katika jamii.

Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, Mhashamu Methodius Kilaini alisema kuwa kujiuzulu ni jambo la kawaida na kumtolea mfano Mzee Ali Hassan Mwinyi kwamba aliwahi kujiuzulu uwaziri na baadaye akachaguliwa kuwa Rais wa Tanzania… “Kujiuzulu ni heshima siyo aibu… hili jambo mawaziri wote wanatakiwa kulitambua.”

Alisema kama ndani ya wizara imeibuka tuhuma na ikathibitishwa kinachofuata ni watendaji wakuu wa wizara husika kuachia ngazi.

Akizungumzia kitendo cha kupishana kwa kauli kati ya Waziri wa Viwanda na Biashara na wa Uchukuzi dhidi ya manaibu wao alisema, “Walitakiwa kuzungumzia tofauti zao katika vikao vya chama chao, siyo kujikosha katika vyombo vya habari.”

Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Mussa Salum aliwataka mawaziri hao kuacha kujitetea katika mambo ambayo yanaonekana wazi kuwa yanawahusu.

“Hakuna sababu ya waziri kuanza kujiteteta katika jambo ambalo anaonekana wazi kuwa anahusika na ndiye mtendaji mkuu wa wizara yake,” alisema Sheikh Salum

Alisema mawaziri hao wanatakiwa kujiuzulu ili kulinda heshima zao huku akiwataka Watanzania kuwa na utaratibu wa kuwajibika pale wanapoona mambo hayako sawa.

Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (Tec), Askofu Yuda Thadei Ruaichi alisema: “Kama mtu umefanya mabaya kwa nini uendelee kung’ang’ania? Sisi tutakachokifanya ni kuwashauri watu kuhusu suala hili ila waondoke kama tuhuma zao zipo wazi.”

Mchungaji wa Kanisa la Maombezi, Antony Lusekelo alisema taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), inaleza wazi hivyo hakuna haja ya mawaziri hao kusita kuwajibika.

Alisema mawaziri hao wanatakiwa kuwajibika kabla ya Watanzania kuamua kuingia mtaani na kufanya maandamano… “Wakati ule wa Richmond kuna ambao waliwajibika. Sasa hawa wanasita kufanya hivyo kwa misingi ipi? Ukimya wao unaipa wakati mgumu CCM.”

Kamati yamshukia Maige

Katika hatua nyingine Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira imependekeza kuwajibishwa kwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Ezekiel Maige kwa madai ya kutengeneza mazingira ya rushwa katika ugawaji wa vitalu vya uwindaji.

Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake, James Lembeli pia imependekeza Balozi wa Tanzania nchini Uganda, Ladislaus Komba achukuliwe hatua za kinidhamu kwa kutoa vibali vya kusafirisha wanyama hai kwenda Pakistan kinyume cha sheria.

Wakati akitoa vibali vya kusafirisha twiga wawili, viboko wawili na swala wanne kwenda Karachi, Pakistan mwaka 2010, Balozi Komba alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.

Akisoma taarifa ya kamati hiyo bungeni jana, Lembeli alisema kamati yake pia inataka watumishi wote wa wizara hiyo waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kashfa hiyo nao washtakiwe.

Lembeli alisema ugawaji wa vitalu vya uwindaji ulitawaliwa na dosari nyingi ikiwamo waziri mwenye dhamana kutangaza majina ya waliopata vitalu bila kuonyesha ni vitalu vipi walipewa na kampuni zisizo na sifa kupewa vitalu hivyo.
Mwenyekiti huyo alisema kampuni tatu, Mwanauta and Company Ltd, Kawawa Hunting Safaris Ltd na Malagarasi Hunting Safaris ziligawiwa vitalu kinyume na mapendekezo ya kamati ya ushauri kwamba zisipewe vitalu kwa kuwa hazina sifa.

Katika tuhuma hizo, kamati hiyo imebainisha kuwa Waziri Maige ambaye pia ni Mbunge wa Msalala, Shinyanga azipatia vitalu kampuni 16 ambazo hazikuomba na vingi vya hivyo vikiwa ni vya madaraja ya kwanza na pili.

Lembeli alisema dosari hizo ziliathiri dhana ya uwazi na misingi ya utawala bora na kuashiria kuwapo kwa rushwa hivyo kusababisha malalamiko kutoka kwa kampuni nyingine zenye sifa ambazo zilinyimwa vitalu.

“Kamati inapendekeza Bunge liitake Serikali kumwajibisha Waziri wa Maliasili na Utalii, Mheshimiwa Ezekiel Maige kwa kutengeneza mazingira ya rushwa ikiwa ni pomoja na kuyanyang’anya vitalu makampuni 16 yaliyogawiwa vitalu bila kuomba,” alisema Lembeli.

Mponda asubiri rungu

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda alisema jana kwamba hatima yake ya kujiuzulu au kuendelea na uwaziri ipo kwa Waziri Mkuu.

Dk Mponda alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari juu ya taarifa za kuwa mmoja wa mawaziri wanaotakiwa kuachia ngazi. Alikuwa akizungumza nao kuhusu maadhimisho ya Wiki ya Chanjo na Malaria Duniani.

Alisema amepokea taarifa hizo za kuwa mmoja wa mawaziri wanaotakiwa kujiuzulu na lakini anasubiri uamuzi wa bosi wake.

Mkono asaini

Juzi usiku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) na Mbunge wa Musoma Vijijini, Nimrod Mkono, juzi usiku alisaini fomu ya majina ya wabunge wasiokuwa na imani na Waziri Mkuu yanayokusanywa na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto kabwe.

Zitto alikuwa akikusanya saini za wabunge wasiopungua 70 ambao ni asilimia 20 ya wabunge wote ili awasilishe hoja ya kutokuwa na imani na Waziri Mkuu kwa Spika wa Bunge.

Mkono alikuwa ni mbunge wa 74 na wa sita wa CCM kati ya 76 waliosaini fomu hiyo hadi jana mchana. Juzi usiku, Mkono alimpigia simu Zitto na kumtaka ampelekee fomu hiyo ili aweke saini yake.

“Mimi ni mjumbe wa NEC na nimepata nafasi hiyo kwa kuchaguliwa na wabunge wenzangu wa CCM, sasa ninapoona wabunge wenzangu wakiwemo wa CCM wanalalamikia utendaji wa mawaziri wetu kwa kuhusishwa na ufisadi wa fedha za umma na Serikali inakaa kimya ni lazima nichukue hatua,” alisema na kuongeza:

“Mawaziri wetu hata wafanye kosa gani sisi wabunge hatuwezi kuwawajibisha, ni mmoja tu naye ni Waziri Mkuu ambaye tunaweza kufanya hivyo. Sasa tumeona kuna mawaziri wamekutwa na kashfa mbalimbali na bado wanang’ang’ani kubaki kwenye nafasi zao hatuna jinsi, ili kuwang’oa nilazima tumuondoe Waziri Mkuu.”

“Sina tatizo na Pinda katika utendaji wake wa kazi lakini hatuwezi kuwaondoa mawaziri wenye kasoro bila ya kumwondoa yeye kwa mujibu wa sheria zetu, ndiyo maana nimesaini fomu hii kwa maslahi ya taifa langu.”

Wabunge CCM wanena

Baadhi ya wabunge wa CCM wametaka mchakato wa kuwang’oa mawaziri uende mpaka kwa watendaji wengine wa Serikali kwa kuwa ndiyo wahusika wakubwa wa matumizi mabaya ya fedha za umma.

Wabunge hao walitoa kauli hiyo jana katika kipindi cha Jambo Tanzania kinachorushwa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Pia walipendekeza kutungwa kwa sheria itakayowajumuisha mawaziri na watendaji wakuu wa wizara na idara zinazotuhumiwa katika makosa ya uhalifu.

Mbunge wa Kalenga, Dk William Mgimwa alisema: “Hii siyo njia pekee ya kupambana na vitendo vya ubadhirifu serikalini lakini lazima tuanze na hatua hii ya kuwawajibisha mawaziri sababu ndiyo njia pekee ya kurejesha imani ya Serikali kwa wananchi.”

Mbunge wa Kisesa, Luhaga Mpina alitaka hadi kufikia kipindi cha Bunge kupitisha bajeti, watendaji wa Serikali wanaotumiwa na matumizi mabaya ya Serikali wawe wamechukuliwa hatua.

Alitaka makatibu wakuu wa Wizara na idara za Serikali, wakurugenzi wa miji na halmashauri za wilaya zinazotuhumiwa kwa ufisadi, kabla ya kikao cha Bunge la Bajeti la Juni, mwaka huu wawe wamechukuliwa hatua.

Imeandikwa na Fidelis Butahe, Geofrey Nyang’oro, Dar; Edwin Mjwahuzi, Masoud Masasi na Daniel Mjema, Dodoma

JUNIOR NAKOZ NA BRAND NEW SONGS KUTOKA A TOWN.

April 23, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.

Junior Nakoz the Street Dogz.
Junior Nakoz the Street Dogz from Ololoo area pande za Ara Moko hip hop city North Tzee!!Kundi linaundwa na Mc;s watatu akiwemo "Yung G",LP", na "Junior",Hizi ni release ambazo ziko hewani officially, na round hii mpango mzima ni audio release kadhaa huku mchakato wa video unaendelea!Tuko Pande za DSM kibiashara,watu wetu wa karibu big up sana kwa support mnazotupatia.

MOPLUS NA LAVOSTI, NGOMA MPYA "Siku Nyingi"

All rights reserved to Asili Yetu.

 Moplus aka Baba wa ukoo na Rasta Lavosti wanakupa brand new joint inayokwenda kwa jina Siku Nyingi,Pini limeundwa na defxtro pande za noizmekah.com,Concious music kwanza for the betterment of our youth and society,elimika & enjoy tha joint!!!!


ORAINE KUTOKA (Effect Zero) AMEDROP NEW SONG (Over That)

All rights reserved to Asili Yetu.

Doraine na Dj Mido (kushoto) Mwanadada Doraine,ni femcee toka arachuga na anadrop first track yake alorekodia pande za noizmekah.com chini ya defxtro.na hapa amemshirikisha DjMido wa kambi ya JamDropa Dj's,,Doraine ni member katika female group inayofahamika kama Effect Zero ambayo ipo katika race za kurecord album yao.
"game la music 2meweza kulisoma poa and hopefully me and ma girl Simaloi as EffectZero,we gwan rock the scene this year,we have faith in our management; Batoo Ent & the JamDropa deejays,our producers and most of all our fans"asema mwanadada Doreine.

KWAITO MPYA (Loop It) 'Rudbwoi Batoo', SPECIAL KWA KUPART

April 21, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.

Rudbwoi Batoo Pata kusikiliza kwaito jipya la Rudbwoi Batoo toka pande za Chuga town,ikiwa ni noizmekah.com exclusive kwaajili ya party goers wote Tanzania. Hii pia ni kwa hisani ya JamDropa Deejays,Dj Mido & Deejay P..Projects zetu kama kawaida zinaendelea,nikiwa kama event organizer ningependa kutoa big up kwa Hip hop City a.k.a ChugaTown kwa kusupport wasanii wao kila 2napoandaa jam session pande zetu!!! 

Hii kwaito ni project ya kwanza katika Jam Dropa Riddim Vol 1,ambayo inasimama kwa ukaribu zaidi na "Batoo Entertainment" ,Artist yeyote atakaye feel kurecord kwenye this beat awasiliane nasi kupitia page yetu ya "Batoo entertainment" katika facebook kisha 2tamtumia beat kwaajil ya kurecord!! Much respect kwa media zote including websites & Blogs,Jaaaaaah blesssss!!!

'QUALITY BROTHERS' NI WIMBO MPYA KUTOKA KWA "Slaiyank"

All rights reserved to Asili Yetu.
 Slaiyank the Quality Brother aunga mkono campaign za kukomesha beto pande za ChugaTown,hii ni ngoma ya tatu ninayo release katika kutambulisha ujio wa album yangu ya "Kilicho bora",na single hii kaunda Defxtro pande za noizmekah.com,Track inaitwa Quality Brothers au kifupi "QB". Mategemeo yangu makubwa ni kuweza kuelimisha jamii kupitia muziki wangu na mimi kama Mc nasimama kama mfano kukanya fikra potofu kuwa ubabe na fujo ni ujanja,Music unakosa support kubwa sana kwa itikadi hizi maana kama ni ajira halafu tunawakosea mashabiki heshima je tutakula wapi!?

WAKAZI WILAYANI BABATI WAKERWA NA TOPE PAMOJA NA MAJI YALIYOTUAMA STENDI YA MABASI MJINI HAPO.

April 20, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.

 Leo nimepata nafasi ya kuutembelea mji huu wa Babati, kwani nimekuwa nikiusikia kwa takribani miaka kadhaa. Wakazi wa Babati wanajitahidi katika swala zima la kilimo na maendeleo yao binafsi.

Stand kuu ya mji wa Babati ikiwa imefurika maji na matope.
Wilaya ya Babati ni moja kati ya wilaya zilizopo katika mkoa wa Manyara. Wakazi wa mji huo hushughurika na shughuri mbali mbali zikiwemo za kilimo na biashara ndogo ndogo.Wakazi wa mji huo wa Babati wanaonekana kukerwa sana na kituo chao kikuu cha mabasi yaendayo mikoani hasa wakati huu wa mvua. Baadhi ya wakazi nilioongea nao wamedai kuwa stand hiyo hujaa maji na tope wakati wa mvua.Na nilipowauliza kuhusiana na serikali inalichukuliaje swala hilo, walisema kuwa imepanga kuhamisha kituo hicho na kujengwa sehemu nyingine, kitu ambacho kinasubiliwa bila siku hiyo kufika. Hata hivyo kutokana na hali ya hewa kuwa ni ya mvua nyingi, juhudi zangu za kuonana na uongozi wa mji huo wa Babati uligonga mwamba.

Hivi ndivyo hali ilivyo katika stendi kuu ya wilaya ya Babati.
Uwanja wa mpira wa Babati ukionekana kujawa na majani.
Chuo cha ualimu kilichopo wilayani Babati cha EVIDA MONTESSORI.
'CANDLE LIGHT' BRAND NEW SONG FROM (Mirry Candle)

April 19, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.


 Mwanadada MirryCandle anayewakilisha pande za Kijenge Arachuga, anadrop brand new video ya "CandleLight" ambayo imetengenezwa na mtu mzima Benjamin wa Mambo Jambo, Audio ikiwa ni kazi toka kwa Samtimber Jumper pande za Fnouk Studios Arusha, Kazii hii ni mojawapo kati ya zingine nnne ambazo mwanadada amerecord, stay tuned for more and more.


'MY CITY' WIMBO MPYA KUTOKA KWA Vatoloco Ft. Jeezy Mabovu & JCB.

All rights reserved to Asili Yetu.


Mambo vip mdau wa music,hii ni kazi mpya kabisa ya jamaa wanaokwenda kwa jina la vatoloco,maskani yao ikiwa Arusha pande za erboru,hii ki kazi yao inaitwa MY CITY,wakiwa wamewashirikisha ,jcb,ibra da hasla na geez mabov,kazi imefanyika ktk studio iitwayo FNOUK STUDIOS ARUSHA,prodyuza akiwa ni samtimber,
 TUNAOMBA USHIRIKIANO WENU.

'BARUA KWA MAMA' BRAND NEW SONG..."ANAPITA"

All rights reserved to Asili Yetu.
Anapita, msanii wa miondoko ya AfroFusion anayewakilisha chuga kaskazini mwa Tz,sasa aja na "barua kwa mama" alorekodi pande za noizmekah.com kwa defxtro,asema "wimbo huu nimeuandika kutokana na maisha ya mjini jinsi yalivyo, vijana wengi tumekuja kutafuta na mama zetu wako mbali na sisi, kwa jinsi maisha yalivyo wakati mwingine mshiko wa kumpigia mother hauna, na wakati mwingine mama mwenyewe kijijini hana simu mpaka kwa jirani,kuna wakati hawa wamama hudhani kwamba tumewasahu halafu huku mjini tunakula bata lakini si kweli, ni utaftaji hapa na pale changanyia na panda shuka ya  gharama halisi ya maisha, pia kuna marafiki ambao kwa bahati mbaya mama zao washatangulia mbele za haki, nao hufikiria kuandika barua.Nawapenda mama zetu wote duniani kwasababu natambua umuhimu wao.Amani tele...

PICHA ZA WASHINDI NA WADAU WA TUZO ZA KILIMANJARO TANZANIA 2012

Mdau wa muziki nchini, muda mfupi baada ya kuwasili katika tuzo za "Kilimanjaro Tanzania Music"  akiwa ni mmoja kati ya wadau maalum walio alikwa katika tuzo hizo.
Ali Kiba akiwa na dada yake pembeni wakati alipo twaa tuzo ya wimbo bora wa zuku rumba..."Dushelele"
Roma akiwa na Izzo B baada ya kuchukua tuzo ya wimbo bora wa Hip hop na baada ya muda mfupi pia alinyakua tuzo ya msanii bora wa Hip hop.
Diomond akitoa shukurani za dhati kwa familia yake pamoja na mashabiki wake baada ya kukabidhiwa Tunzo kutoka kwa msanii Chid Benzi.Diomond aliongoza kwa kupata tuzo tatu.
Gadna G Habash akimuwakirisha mkewe Lady Jay dee wakati wa kupokea tunzo yake.
Adam Mchonvu a.k.a Baba Jonii akijiandaa kumpatia tuzo msanii Barnabar
Barnabar akitoa shukurani baada ya kukamata tuzo yake.
Khadija Kopa
Isha Mashauzi (mkurya wa kwanza kuimba taarabu) akimikamata tunzo ya wimbo bora wa taarabu.
Queen Darlin akitoa shukurani kwa mashabiki baada ya kukabidhiwa tuzo ya wimbo bora wa Ragga/dancehall.
Worrier From The East wakiwa wameshikilia tunzo ya wimbo bora wa Rege (Arusha gold).

"Every Where We Go" COLLABO MPYA YA Moplus na JCB .ft. Banx.

April 11, 2012

All rights reserved to Asili Yetu.
 Moplus na JCB wamshirikisha Banx katika brand new collabo iloundwa pande za noizmekah.com,mdundo ukiwa wa producer Mosco na vocal mixing Defxtro,Everywhere we go ni motivational hiphop joint fo all ya'll hiphop fans out there,kwa mujibu wa taarifa zilizowahi kutolewa na MC's hawa ni kuwa hii collabo ni moja kati ya zingine saba ambazo kwa pamoja zitakuwa katika compilation mixtape ya pamoja!!!

HIP HOP MC's NDANI YA COLLABO MOJA YA "Gangstar".

All rights reserved to Asili Yetu.
Pini hili la  "Gangsta",ni collabo kati ya hip hop Mc's anzia Dar-Arusha-Mombasa mpaka Nairobi.Artists walopita ni BouNako, FiDo, MoPlus, Frost ,GeeZMabov, LavosT na RitchieRich,Hip hop ni worldwide na tunafanya kazi kwa pamoja kuimarisha game na mshikamano ambao upo kati yetu wasanii,Geez Mabovu anarepresent Dirty South pande za DSM,FiDo,MoPlus,Frost na BouNako wanarepresent Arachuga,Lavosti toka Ukoo MauMau anarepresent Mombasa na RitchieRich toka HeadBangaz International akirepresent pale Nairobi City,Audio ikiwa imesimamiwa pande za Noizmekah Studios,Video ya pini hili inaendelezwa editing Pande za RED Films Arusha..

"RIGHT NOW" NGOMA MPYA...Banxtramatic na Gnako.

All rights reserved to Asili Yetu.
 Kwa kuanza ,Nitangulize our deepest Sympathies toka Noizmekah Production studios Arusha,May the Soul of the great Film icon "Steven Kanumba" rest in eternal peace,We all head the same path...Banxtramatic aka Hookmaster toka pande za Chuga Town na mtu mzima te kankara aka Gnako wanakuja na banger waloipa jina "Right Now" ikiwa ni 1st solo project ya banx kuwa officially released kwa hewa,Kama inavofahamika wara na banx waliskika pamoja kiping\di cha nyuma kidogo katika pini la Right here alokuwemo pia mzee mzima Umbwa 4rom Watengwa "Nimekuwa quiet kw muda na hii ni tokana na majukumu ya kielimu zaidi na this joint ni exclusive kwa watu wangu wote round the world,mkono ni wa Defxtro pande za noizmekah.com,Peace kwa supporting media zote ndani na nje ya BongoTz!!..once again,Rest In peace to all our lost loved ones!

NEW NEWS TODAY

HABARI ZA MASTAA WA MOVIE

PATA MATUKIO KILA SIKU

Advertisement

Advertisement

GOSPEL NEWS ZOTE ZINAPATIKANA HAPA

YOUTUBE: CHEKI HABARI NA VIDEO HAPA

SIKILIZA HAPA VIPINDI VYETU VYA RADIO

 
© Copyright ASILI YETU TANZANIA 2012 -2013 | BLOG DEVELOPED BY ASILI YETU TZ | PROPERTY OF ASILI YETU TANZANIA.