Header Ads

Breaking News
recent

Sababu zinazopelekea chui kula chakula chake juu ya mti.

 Chui ni mnyama pori anayepatikana katika hifadhi za hapa nyumbani Tanzania na kwingineko Afrika, mnyama huyu ni kati ya wanayama wanao kula nyama ya wanyama wa aina tofauti na wao.

Hata hivyo tabia ya mnyama huyu imeonekana kuwa tofauti kidogo na wanyama wengine wanaokula nyama.

Chui ameonekana kujali sana chakula chake hivyo hataki bugudha kabisa wakati wa chakula, huenda angekua binadamu wangemuita mchoyo au mbanizi wa vitu vyake.

Unaambiwa chui kupandisha kitoweo chake juu ya mti, kunamsadia kuzuia chakula chake kuibiwa, hii ni kwamujibu wa utafiti uliofanywa mwezi Februari mwaka 2017.

Utafiti uliofanywa na shirika moja lisilokuwa la serikali uligundua kuwa chui katika mbuga ya Sabi Sands nchini Afrika ya kusini huwawinda karibu familia 40 ya wanyama.
Chui hupandisha mtini nusu ya wanyama anaowawinda. Pia hupoteza moja ya mawindo yake kati ya matano kwa wanyama wengine kama fisi, simba na hata chui wa kiume.

Ikiwa chui ataamua kupandisha mtini windo lake na kisha kugundua hakuna mshindani karibu anaweza kuburuza kitoweo kutafuta mti unaofaa ulio karibu.

Mara chui anapokaribia mti hupanda hadi umbali wa mita10 juu kutafuta eneo lililo salama kuning'iniza windo lake.

Hata hivyo wakati mwingine hali huwa ni ya dharura. Kama fisi yuko karibu Chui mara moja anaweza kupanda mti wowote ulio karibu kuzuia chakula chake kuibwa.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.