Header Ads

Breaking News
recent

Tips za Afya kwa Wanawake kwaajili ya Moyo, Akili na Mwili mzima

Kuwa na afya njema katika maisha ni jambo ambalo ni ndoto kwa kila binadamu anayehitaji kuendelea kuishi. 

Asili yetu Tanzania kupitia kona ya AFYA BORA tunaangazia afya kwa kinamama ambao pia ndio walezi wakuu katika familia zetu. Dondoo zifuatazo zinaweza pia kutumika na mtu wa jinsia tofauti na ya kike:-

1. Fuata mlo bora kwa Afya ya moyo wako

Kuna mapishi rahisi ikiwa lengo lako ni kuyaweka mbali matatizo kama vile ugonjwa wa moyo na viharusi.
 • Kula matunda kwa wingi na mboga za majani
 • Chagua kula nafaka kwa ujumla. Jaribu mchele wa kahawia badala ya mchele mwenyeupe.  
 • Chagua vyakula vyenye protini kama vile kuku, samaki, maharagwe na mboga za majani. 
 • Punguza kabisa kula vyakula vilivyoandaliwa kwa sukari, chumvi, na mafuta mengi.  
2. Fanya Mazoezi Kila Siku

Mazoezi huongeza afya ya moyo wako, hujenga nguvu za mifupa na misuli, na kuondoa matatizo ya  afya.

Kitaalamu unashauliwa kuwa na lengo la masaa 2 na nusu ya kufanya shughuli za wastani, kama vile kutembea kwa haraka au kucheza kila wiki. 

Ikiwa uko sawa na mazoezi ya nguvu, tenga saa 1 na dakika 15 kwa wiki, kama vile kukimbia au kucheza michezo mbali mbali. Ongeza siku kadhaa za mafunzo ya nguvu, usiishie hapo.

3. Punguza Uzito

Unapopunguza uzito hupunguza pia hatari ya kupatwa na ugonjwa wa moyo, ugonjwa wa kisukari cha aina 2, na kansa. 

4. Mtembelee Daktari wako
 
Pata ukaguzi wa mara kwa mara. Daktari wako ataendelea kufuatilia historia ya matibabu yako na anaweza kukusaidia kukaa na afya bora. 


Kwa mfano, ikiwa uko katika hatari ya ugonjwa wa osteoporosis, hali ambayo inafanya mifupa kuwa dhaifu, anaweza kukushauri kupata calcium zaidi na vitamini D. 

5. Punguza Msongo wa Mawazo
 
Msongo wa mawazo unaweza kukughalim pesa kwenye afya yako. Labda hauwezi kuepuka kabisa, lakini unaweza kupata njia za kupunguza athari hiyo. 


Usiwa mtu wa kuchuachukia sana. Jaribu kuweka mipaka wewe mwenyewe na watu wengine.Jifunze kusema hapa. 

Kuondoa Stress/msongo wa mawazo>>>
 • Shiriki mazoezi
 • Kula kwa afya
 • Piga soga/stori na marafiki
 • Shiriki mazoezi
 • Jiweke bize
 • Shiriki massage
 • Ongea na ndugu jamaa na marafiki
 • Usiumie na tatizo, liweke wazi kwa mtu unayemuamini ili akupe ushauri
 • Tumia mitandao ya kijamii, Facebook, Instagram, WhatsApp nk.
 • Angalia movie na kusikiliza muziki kama wewe ni mpenzi wa vitu hivi, ila usiangalie au kusikiliza vitu vya kuhuzunisha kwani vitaendelea kuchochea msongo wa mawazo kwako. 
6. Unda Tabia ya Afya

Ukifanya maamuzi sahihi leo, unaweza kuepuka matatizo ya kesho.
 • Piga mswaki kila siku na fanya hivyo kila siku na ikiwezekana piga mswaki hata baada ya kula
 • Usivute sigara
 • Pungunza unywaji wa pombe, ikiwezekana kunywa mara moja tu kwa siku au ikiwezekana achana nayo kabisa (kwa mnywaji wa pombe) 
 • Kama unadozi ya kumeza dawa, basi zingatia maelekezo uliyopewa na daktari
 • Boresha usingizi wako. Lala kwa masaa 8 kila siku (usiku) na kama unatatizo la kukosa usingizi basi ni vyema ukamuona daktari
 • Ota jua asubuhi na usiote jua la kuanzia saa 4 hadi saa tisa
Kila siku jaribu kuwekeza katika afya yako, hakika utakuwa ni mwenye afya bora na utaishi maisha ya ndoto zako. Karibu tena katika ukurasa mwingine wa Afya Bora ya Asili Yetu Tanzania.

No comments:

KARIBU UTOE MAONI YAKO HAPA

Powered by Blogger.